Na Mwandishi Wetu, Mbeya

Mtuhumiwa katika kesi ya wizi wa simu, Endrew Festo (28) safiri ya maisha yake ilifika tamati baada ya kuswekwa lupango na kuaga dunia.

Mtuhumiwa huyo mkazi wa Mbalizi Shigamba amefariki dunia Agosti 16 mwaka huu usiku akiwa ndani ya kituo cha polisi Nzovwe mkoa wa Mbeya.

Shuhuda wa tukio hilo wameiambia Morningstar POST kuwa mtuhumiwa huyo alifikishwa kituoni akiwa amepigwa baada ya kutuhumiwa kuiba simu ya mkononi na kuwekwa mahabusu.

Hata hivyo, mtuhumiwa huyo hakuweza kufika asubuhi ya siku ya pili alikutwa tayari mauti yamemfika.

Ndugu wa marehemu wana mpango wa kuandamana hadi kituo cha Polisi cha Kati Mbeya kujua sababu kwa nini mtuhumiwa amefia ndani ya kituo cha polisi bila kupelekwa hosptali.

Wanasema kuwa polisi wanamshikilia mtu mmoja anayedaiwa kuwa alihusika kumpiga mtuhumiwa huyo.

Hata hivyo nduguĀ  wanasema kuwa kifo cha mtuhumiwa huyo kinatokana na uzembe wa polisi kwa kuwa wangeweza kumwaisha hosptali pengine maisha yake yangeweza kuokolewa na madaktari.

Kamanda wa Polisi Mkoa Mbeya hakuweza kupatikana na mara moja kuzungumzia tukio hilo.

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Wambura

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *