Na Jones Mwangónda
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan, umeanza mwanzo mzuri wa utawala wako kwa kuunganisha wanasiasa wote nchini na kurudisha demokrasia nchini kwa kuruhusu mikutano ya hadhara ya wanasiasa wa upizani iliyopigwa marufuku na mtangulizi wako hayati, Dkt. John Pombe Mgufuli na hivyo kusisimua upya siasa za nchi yetu zilizosinzia kwa takriban miaka mitano. Leo tunashuhudia vyama vya upinzania vikiendesha siasa zao kwa uhuru na amani.
Kwa upande mwingine, ameongea na makundi mfano, wafanyabiashara, wakulima na wafanyakazi na kuahidi kutatua kero zao sitakazowezekana ili kuboresha shuguli zao kama njia moja wapo ya kuharakisha maendeleo ya nchi yetu kwani Rais Samia anaamini watu wakianza safari pamoja wataimaliza pamoja badala ya mtu mmoja akiwa na kasi kubwa kuliko wenzake safari inaweza kuwa na mashaka.
Rais Samia amerekebisha baadhi ya taasisi za serikali na zingine kuziunganisha ili kuzipa nguvu na kubana matumizi yaliyokuwa yanalalamikiwa na wengi na kupunguza kwa kiasi kikubwa utawala wa mabavu na kuwataka Watanzania waheshimu utawala wa nchi, lakini pia kuimarisha nidhamu ya kweli badala ya kuwa na nidhamu ya woga na pia aliwataka viongozi wenzake wapunguze ukali na waongoze na watoe maelekezo ya staha kwa wanaowaongoza.
Rais Samia anaamini mtu akielezwa kwa ulimi laini ateelewa zaidi na kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha. Rais Dkt. Samia pia amepanga safu yake anayoiamini kuwa utamsaidia kutekeleze majukumu atakayowapa kwa uhakika na ukweli akinyofoa uongozi pande zote mbili za muungano na kutekeleza tamko la umoja wa kimataifa la usawa wa jinsia katika uongozi wa kuwapa wanawake nafasi nyeti za uongozi wa nchi zikiongozwa na yeye mwenyewe kuliko rais yeyote aliyewahi kutawala nchi hii na Afrika kwa ujumla na hata dunia nzima inakadiriwa asilimia zaidi ya 35 viongozi ni wanawake.
Hata Ulaya, Asia na Marekani sidhani kama wametekeleza usawa wa jinsia katika uteuzi wa viongozi wao unaotakiwa kuwa asilimia hamsini kwa hamsini. Rais Samia kaandika rekodi yake ya dunia hii kwa vizazi na vizazi kumkumbuka.
Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kujenga msingi imara katika nyanja mbalimbali ameanza kupandisha uchumi wa Tanzania kwa kutafuta wawekezaji wenye mitaji kwenye maeneo ambayo yana changamoto, mfano kwenye bandari zetu.
Kila mtu anajua kuwa bandari ni kitovu cha uchumi wa Tanzania lakini bandari hizi hazina ufanisi. Sasa kupata wawekezaji wenye mitaji mikubwa kama DP World kutoka Dubai. Haikuwa rahisi kuwapata isipokuwa kwa ushawishi mkubwa aliokuwa nao rais wetu na wasaidizi wake mpaka serikali ya Dubai na Tanzania kuingia mikataba ya nchi na nchi na sasa mchakato ya kisheria inaendelea na itakapokamilika tutashuhudia uwekezaji mkubwa wa bandari zetu na utakuwa na mchango mkubwa wa ukuaji wa uchumi na kutuletea maendeleo ya haraka.
Mama tambua, unapokomboa watu ujue kuna watu wachache waliokuwa wanafaidika na bandari hizi. Hao watapinga sana uwekezaji huu lakini tulio wengi tunakuunga mkono. Mama tuko nyuma yako na tuko imara kukutetea wewe wakati unakomboa Watanzania.
Watu wasioitakia mema nchi yetu ndio wanapiga kelele kwa maslahi yao binafsi na watu walio nyuma yao.
Rais wetu umekuwa muwazi kwenye muchakato huu na hatujawahi kuona Bunge la Jamhuri ya Tanzania likijadili mikataba kwa uwazi kama kwenye utawala wako. Mama kanyaga twende tuimarishe uchumi wa nchi yetu.
Mungu ibariki Tanzania.
Mwandishi wa Makala haya anapatikana 0766 600 909
Rais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan