Na Mwandishi Wetu, Mbeya
WAKULIMA wamepewa misamaha ya kodi katika uagizaji wa trekta, kitalu nyumba, mbolea pamoja na pembejeo za kilimo.
Ofisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), mkoa wa Mbeya, Nicodemas Massawe ameeleza hayo katika maonesho ya nane nane yanayondelea katika viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya.
“Kwa hiyo wale wote ambao ni wakulima wadogo, wa kati na wakubwa watembelee banda letu ili wajue ni vitu gani vimesamehewa kodi na ni kiasi gani ili anapoagiza hizo zana kwa ajili ya kuboresha kilimo iwe rahisi kwake na mwisho wa siku kilimo kiwe na tija,” amesema.
Amefafanua kuwa sheria yao pia inamtaka mkulima anayelima kibiashara kulipa kodi ya mapato.
“Mkulima anayepaswa kulipa kodi ni yule ambaye kwa mwaka thamani yake ikiwa inafikia sh milioni nne na kuendelea lakini chini ya hapo anasamehewa,” amesema.
Kwenye vyama vya ushirika vya kilimo alisema wanapaswa kulipa kodi kutokana na faida iliyopatikana kwa mwaka.
“Lakini sheria yetu ya kodi ya mapato imeweka utaratibu kuwa chama chochote cha ushirika ambacho mapato ghafi yake hayazidi milioni 100 kwa mwaka nacho kimesamehewa kodi ya mapato,” amesema.
Waziri wa Kilimo Bw. Hussein Bashe