Na Jones Mwangónda
Katika Maisha yetu ya kila siku, vinywaji vyetu vingi vimewekwa kwenye chupa za plastiki jambo ambalo wataalamu wa afya wanadai kuna madhara makubwa ya baadae katika maisha ya binadamu. Wanaeleza kwamba ni jambo la muhimu ufahamu wa madhara hayo uwafikie watumiaji au walaji ili waweze kuchukua uamuzi sahihi kwa ajili ya afya zao kwa sasa na baadae.
Makala haya inatoa ufafanuzi kuhusu madhara yatokanayo na matumizi ya vinywaji vilivyomo kwenye chupa za plastiki. Vilevile, itatoa ushauri kuhusu nini kifanyike kwa ajili ya afya bora lakini sio bora maisha.
Kuchuuruzika kwa kemikali
Sio siri kwamba maji na vinywaji vingine yaliyomo kwenye chupa za plastiki ni hatari katika maisha ya binadam. Utafiti unaeleza kwamba kemikali kama BPA na phthalates zinaweza kuchuruzika kwenye vinywaji vilivyomo kwenye chupa hizo za plastiki. Na hii inaelezwa ikiwa vinywaji hivi zimehifadhiwa sehemu ya joto ama kutumika kwa mda mrefu.
Utafiti inaonyesha kwamba uhusiano kati ya kemikali hizo na vinywaji zinaweza kuleta madhara makuu matatu mwilini.
Kwa usalama kutokana na madhara hayo, watu wengi wanaombwa kupunguza ama kukomesha matumizi ya chupa za plastiki, vikombe na sahani. Ni muhimu kuuliza kama ni salama kutumia vyombo hivyo kabla ya matumizi.
Kuathiri ukuaji wa ubongo
Kuathiri ukuuaji wa ubongo ni moja wapo ya hatari kutokana na utafiti wa wataalamu wa afya.
Utafiti wa hivi karibuni unaeleza ugunduzi wa kutisha wa jinsi vinyemelea vya plastiki na jinsi vinavyojipenyeza na kuingia kwenye vyakula vyetu. Hali hii inaleta hatari kubwa kwenye ukuaji wa ubungo kwa watoto wetu ambao ubongo wao baado unakuwa. Plastiki hizi zinatoka katika vyanzo na mazingira hatarishi na vifungashio ambavyo kwa ujumla wake ni hatarishi kiafya.
Ni muhimu ifahamike kwamba utafiti kuhusu jambo hili bado unaendelea lakini kwa sasa ni muhimu watunga sera watilie manane swala hili kuokoa jamii yetu na janga hili.
Kupunguza au kuondoa kabisa matumizi ya plastiki ni jambo jema kabisa ili watoto wetu ambao ubungo wao bado unakuwa wasikumbwe na janga hili kwa ajili ya manufaa ya watu wachache.
Njia mbadala
Kwa kuzingatia athari ya matumizi ya plastiki, ni muhimu serikali zetu na wadau husika kubuni njia zingine mbadala wa vyombo vya kunywea maji. Bahati nzuri, kuna njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kunusuru walaji na janga hili.
Matumizi ya vyombo vya kioo – Kioo haivujishi kemikali kwenye kinywaji. Hii njia pia ni ya kudumu, kuruhusu matumizi ya zaidi na zaidi na vile vile kuna urahisi katika kusafisha chombo husika.
Matumizi ya vyombo ya chuma zisizoota kutu (Stainless steel bottles) – Vyombo hivyo havina madhara yoyote kwa vile ni “non-reactive” haina mahusiano ya kuchangamana na kinywaji iliyomo ndani yake na hivyo basi ina hakikisha usalama wa kinywaji kwa mutumiaji. Vyombo hivyo pia ni imara na kudumu kwa muda mrefu, sio vizito na vinaweza kubeba kinywaji baridi au moto kwa mda mrefu.
Kwa ujumla, kunywa vinywaji kupitia vyombo vya plastiki kuna athari kubwa sana za kiafya, hii ni kutokana na kuchuruzika kwa kemikali kutoka kwenye chupa ya plastiki na kuingia kwenye kinyawji. Hali hii inendelea kuhatarisha maisha ya walaji. Njia pekee sasa ya kuepuka athari hizi ni kufikiria matumizi ya vyombo vya vioo au vyombo zilizotengenezwa na vyuma zisizoota kutu (stainless steel).
Uamuzi mwafaka katika jambo hili itapunguza kemikali hatarishi zinazochuruzika na kujipenyeza kwenye miili yetu. Vile vile itasaidia kutoa plastiki kwenye mazingira yetu na kuepukana na uchafuzi wa mazingira.
Chupa za plastiki