Na Mwandishi Wetu
Vijana 1,000 watanufaika na ufadhili wa mafunzo ya ujuzi yatakayotolewa kwenye vyuo vya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta), ikiwa ni hatua za kukabiliana na changamoto ya ajira nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, amesema jana Julai 20, 2023 wakati akisaini mkataba wa ufadhili wa mafunzo hayo na uongozi wa VETA.
Sabi alisema suluhisho la ukosefu wa ajira nchini ni kutengeneza mazingira bora yatakayowezesha vijana wengi kujiajiri, kwenye ajira stahiki zitakazowawezesha kujipatia kipato.
“Jambo hili litawezekana kupitia shughuli za ufundi stadi, shughuli kwenye sekta ya teknolojia ama shughuli zinazohusu ubunifu na mengine. Mafunzo yatakayowawezesha vijana kuwa mahiri katika maeneo haya ndio mkombozi wa tatizo la ajira kwa vijana,”amesema.
Alisema ndio maana kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wameamua kuanzisha mpango wa ufadhili wa ufundi stadi kwa vijana kupitia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo Stadi (Veta).
Sabi alisema mpango huo unajulikana kwa jina la NBC Wajibika Scholarship, ambao utalenga kutoa ufadhili kwa vijana 1,000 na kwamba wametenga shillingi milioni 100 kwa kuanzia.
Amesema kupitia fedha hizo watafundishwa masomo ya ufundi ujenzi, ushonaji, useremala, upambaji na mengineyo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amewataka kutokuwa na hofu kwa sababu fedha hizo zitatumika kwa uadilifu na kwa uwazi.
“Na sisi vitabu vyetu vitakuwa wazi muda wote kuona utaratibu ambao tutautumia. Lakini tungependa utaratibu huu uwekeze katika fani moja ikiwezekana chuo kimoja ama viwili, tuweze kupima matokeo makubwa kwa miaka miwili ama mitatu,” amesema.
Wanafunzi wa chuo