Na Mwandishi Wetu
Kigogo mmoja anayefanya kazi Chuo cha Kodi kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam, (jina tunalihifadhi kwa sasa), anadaiwa kukiuka sheria za ujenzi na ukwepaji wa kodi.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa Morningstar POST, kigogo huyo, anadaiwa kujenga mradi wa ujenzi wa jengo la biashara la ghorofa mbili, maeneo ya Mbezi Kwa Yusufu la zaidi ya thamani ya milioni 500 bila kutumia wakandarasi.
Inadaiwa kuwa kigogo huyo amekwepa kodi mbalimbali kwenye mradi huyo.
Kwa mujibu wa bango la ujenzi lililowekwa kwenye mradi huyo, Mkandarasi aliyeorodheshwa hana mkataba na kigogo huyo na kampuni yake haina uwezo wa kujenga jengo lenye thamani ya milioni 500 licha ya kuwa limewekwa katika mradi huo kama ndio mkandarasi anayesimamia ujenzi.
Hata hivyo, bango la ujenzi lililopo kwenye mradi huu inadaiwa limeibwa na makampuni yaliorodheshwa kwenye bango hilo hawana mkataba na kigogo huyo.
Hata hivyo tunaendelea kuwatafuta wamiliki wa kampuni zilizoorodheshwa kwenye bango lililopo kwenye mradi huo, viongozi wa Bodi ya Wakandarasi (CRB) na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kuzungumzia mradi huo na ukiukwaji huo wa sheria unaofanywa na kigogo huyo.
0713685823
