Na Mwandishi Wetu
Jeshi la Polisi Nchi limekuwa likikamata mafuta ya disel na petrol mitaani mara kadhaa lakini, wachambuzi wa mambo wanajiuliza mafuta haya wanayapataje?
Polisi wamekuwa wakikamata baadhi ya watu wanaouza mafuta ya disel mtaani bila kuwa na vibali mara kadhaa lakini biashara hiyo inazidi kuendelea kwa kasi.
Idadi ya watu ambao wamekuwa wakiongezeka kuuza mafuta ya disel na petro mtaani inazidi kuongozeka hususani katika jiji la Dar es Salaam.
Idadi ya watu wengi wamekuwa wakiuza mafuta ya disel na petrol kwenye ”videbe” na katika mitaa na maeneo ambayo ni hatari kwa uzaji wa mafuta.
Kwa mujibu wa sheria ya mafuta hairusiwi kwa mtu yoyote kuuza mafuta kwenye maeneo ambayo haruhusiwi na yasiyokuwa katika kituo cha mafuta kilichosajiliwa na mamlaka husika.
Uchunguzi wa Morningstar POST umebaini kuwa watu wengi wamekuwa wakiuza mafuta hayo kinyemela mtaani bila vibali.
Uchunguzi umebaini kuwa baadhi ya wafanyakazi wasiokuwa waaminifu kwenye miradi ya serikali na ofisi za serikali wamekuwa wakiba mafuta na kuwauzia wafanyabishara wa mtaani.
Wafanyabiashara hao wa mafuta wamekuwa wakinunua mafuta kutoka kwa madereva na wafanyakazi wa miradi ya serikali kama vile mradi wa ujenzi wa Mwendokasi.
Mradi wa treni ya mwendokasi inayojengwa kutoka jijini Dar es Salaam ambako wafanyakazi wanaiba mafuta na kuwauzia wauzaji wa mafuta mtaani.
Idadi kubwa ya watu wanaouza mafuta ya kiholela mtaani ni pamoja na Buza, Temeke, ambako polisi wamekuwa wakikamata kila mara bila kuchukua hatua na watu hawao wanaendelea kuuza mafuta mtaani.
Askari wa Jeshi la Polisi nchini wakiwa wamekamata mafuta ya “videbe”