Waziri wa Fedha, Balozi, Khamis Mussa Omar, ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato jijini Dodoma, ambapo utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 86.7.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi huo kwa Waziri wa Fedha, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi, Godfrey Kasekenya, amesema ujenzi unaendelea vizuri, huku baadhi ya miundombinu muhimu ikiwa imekamilika na mingine ikiwa katika hatua za mwisho za utekelezaji.

Amesema pia kuwa mradi huo umezalisha ajira 2,117 tangu ulipoanza kutekelezwa, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuimarisha miundombinu ya usafiri wa anga na kuchochea shughuli za kiuchumi nchini.

Katika ziara hiyo, Waziri wa Fedha aliambatana na mwenyeji wake, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi, Mhandisi, Aisha Amour, pamoja na wataalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Ujenzi na Wakala wa Barabara (TANROADS).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *