
Na Mwandishi Wetu
BAADHI ya Sheria za nchi, mila na tamaduni za makabila mbalimbali hapa nchini zinakataza mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja.
Hata hivyo, katika baadhi ya maeneo hasa yale ya mijini, vitendo vya mwanamke kuhusiana kimapenzi na mwanamke mwenzake, ama mwanaume kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwenzake, vimekuwa vikishamiri kwa kasi.
Imekuwa kama utamaduni mpya, lakini utamaduni ambao kwa mila na desturi za Tanzania, kushiriki mapenzi ya jinsia moja ni dhambi ambayo katika familia nyingi mhusika anatengwa.
Hali kama hiyo imemkuta Joyce Mwaijibe, mmoja wa wachezaji nyota wa netiboli ambaye anakiri kwamba mapenzi ya jinsi moja yamevuruga malengo yake ya kucheza mchezo huo, lakini pia kutengwa na familia yake kwa ujumla.
Akizungumza na Mta!dao huu, Joyce mwenye umri wa miaka 22 anasema kwamba kwasasa maisha yake yamekuwa ya kuhangaika huku na kule baada ya familia yake akiwemo mama yake mzazi kuamua kumtenga.
“Ni kweli nimekuwa nikijihusisha na mapenzi ya jinsia moja na siyo jambo la siri. Hata huyo mpenzi wangu (anamtaja kwa jina moja la Sophia) anafahamika kwa kila mmoja, lakini familia imegoma kuona tukiwa na mahusiano. Siwezi kulalamika popote tena, familia hainitaki, na hata nikilalamika serikalini nako hawataki tabia hizi” anasema.
Joyce anasema mama yake aitwaye Suzan, dada na kaka yake wote hawataki kumuona kiasi kwamba sasa amekuwa akiishi kwa majirani na wasamaria wema wengine.
“Kwangu ni shida, nilikuwa na malengo makubwa ya kucheza netiboli nilikuwa na malengo makubwa ya kusoma mpaka nje na sasa nafikiria nifanye nini na maisha haya magumu, na kusema ukweli nawaomna wasamaria wema waangalie namna ya kuniokoa” amesema nyota huyo aliyecheza netiboli kuanzia shule ya msingi, sekondari na kisha timu kadhaa za mitaani wiayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Mama wa nyota huyo Suzan Joseph, mkazi wa Temeke Jijini Dar es Salaam naye amekiri kumtimua binti yake huyo akisema kwamba hakuna familia inayojitambua ambayo inaweza kuruhusu mambo kama hayo.
“Ni kweli nimemfukuza, hata ndugu zangu lakini pia ndugu wa upande wa baba yake nao tumesimamia jambo hili” amesema.