MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Mkoa wa Mwanza umenufaika na zaidi ya shilingi trilioni 5.6 zilizotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Nyamagana, Dkt. Samia alisema fedha hizo zimeelekezwa katika miradi ya kuboresha huduma za kijamii, ikiwemo ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Mwanza hadi Usagara, ambayo itakuwa na barabara ya mwendo kasi katikati.

Aidha, alibainisha kuwa Serikali itaendelea na utekelezaji wa mradi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza–Isaka, ambacho kimefikia zaidi ya asilimia 63 ya ujenzi.

Dkt. Samia aliongeza kuwa kukamilika kwa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kutachochea kwa kiwango kikubwa ukuaji wa uchumi wa jiji hilo, kwa kuwa treni ya mwendo kasi itapunguza muda wa safari kutoka saa 18 hadi saa 8 pekee.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *