NA MWANDISHI WETU

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Heche amesema mpaka sasa hawajui alipo Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu baada ya kukamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma jana.

Akizungumza na waandishi wa habari, mkoani humo, Heche amesema licha ya kupata taarifa ya ujumla ya kukamatwa kwa kiongozi huyo bado hawajajua yupo kituo gani.

“Mpaka sasa hatujaambiwa yuko wapi, hakuna anaejua kutoka kwenye chama chetu kwamba Mwenyekiti wetu yupo wapi” amesema Heche.

“Mawakili wetu mbalimbali ikiwemo Robert Amsterdam tayari tumeshawataarifu na wanafuatilia jambo hili ndani na nje ya nchi, kwa hapa ndani tuna wakili Peter Kibatala, Deogratius Mahinyila na wengine “ amesema Heche.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *