Na Mwandishi Wetu,

BODI ya Chai Tanzania imefanya kikao cha kujadili masuala ya uwekezaji katika Kiwanda cha Mponde kilichoko wilayani Lushoto, mkoani Tanga.

Kikao hicho kilihudhuriwa na mmoja wa wabia wanaounda kampuni ya Mponde kutoka taasisi ya mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF).

Aidha, kiwanda hicho kilieleza changamoto mbalimbali kama vile upatikanaji wa nishati ya umeme ambapo kwa mwezi wanaweza kukaa mpaka masaa 200 hadi 300 bila ya nishati ya umeme hivyo kuzorotesha ufanisi.

Aidha, kiwanda hicho kiliongelea kuhusu uboreshaji wa miundombinu ya barabara ambazo huwa zinasumbua wakati wa mvua na kusababisha kutopata uzalishaji mzuri kutokana na barabara kutopitika kirahisi.

Bodi ya Chai imeahidi kuzungumza na mamlaka husika kwa ajili ya kuona namna ya kutatua changamoto hizo ili kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa Chai kutoka kiwanda hicho.

Chai inayotokana na Kiwanda cha Mponde imekua ikivutia wanunuzi wengi kutokana na utaratibu mzuri wa kuzingatia ubora wa majani ya chai wanayochakata kiwandani kwao.

Menejimenti ya kiwanda hiko imeshukuru Bodi ha Chai kwa kuwasaidia kupata soko la Chai la Oman baada ya jitihada za Bodi kwenda kushiriki katika kongamano la Biashara na uwekezaji lililofanyika mwezi Septemba 2024.

“Tunaishukuru sana Bodi ya Chai kwa kuendelea kutafuta masoko kwa ajili ya kuinua Sekta ya Chai. Leo tunatuma kontena tatu za Chai kwenda Oman na tayari zipo bandarini kwa ajili ya kuondoka” Alisema bwana Muhoja manane Meneja wa kiwanda hiko.

Bodi ya Chai itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha sekta ya Chai in

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *