Na Mwandishi Wetu, WMTH, Dar es Salaam

JUMLA ya Wilaya 139 nchini zitafikiwa na huduma ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na mpaka sasa Wilaya 108 tayari zimefikiwa huku Wilaya 31 zilizosalia nazo zikitarajiwa kupata huduma ya mkongo wa Taifa ifikapo mwezi Juni mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) tarehe 07 Januari, 2025 wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Pwani alipotembelea na kukagua Vituo Vya Mkongo vilivyopo Chalinze, pamoja na kituo kipya cha Mkongo wa Taifa kilichopo Kibaha, Mkoa wa Pwani.

Aidha, Mhe. Mahundi amempongeza na kumshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavvyo endelea kuiwezesha Sekta ya Mawasiliano apa nchini kwa kuendelea kuwekeza fedha nyingi katika Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na kuhakikisha Shirika linakuwa kibiashara pamoja na kuifanya Tanzania kuwa ya kidijitali.

Vilevile, Mhe Mahundi ameeleza kuwa Serikali tayari imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kuelekea Nchi Jirani ya Congo (DRC) kupitia Ziwa Tanganyika hadi Kalemei na tayari. Utekelezaji wake umeshaanza na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2025 mradi huu utakuwa umekamilika.

Sambamba na hayo, Mhe. Mahundi ameeleza kuwa kazi kubwa inaendelea kufanyika katika uwekezaji wa Mkongo wa Taifa ikiwa ni pamoja na kuunganisha Mkongo wa Taifa na Mikongo ya Baharini, kupitia SEACOM, EASSY na 2AFRICA, na kwa kuzingatia tunajenga Tanzania ya kidijitali tunaunganisha Mkongo wa Taifa na Mikongo ya Baharini iliyopo Mombasa Kenya kupitia Horohoro, Tanga. Na hii itasaidia kuongeza uhakika wa huduma ya Mawasiliano nchini.

Endapo mkongo wa Taifa wa Mawasiliano utakamilika utapanua wigo wa kibiashara ndani na nje ya nchi na kuongeza uchumi wa kidijitali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *