BBC

Urusi imesema Ukraine ilirusha makombora ya masafa marefu yaliyotolewa na Marekani nchini humo kwa mara ya kwanza siku ya Jumanne.

Ukraine ilitumia makombora ya Atacms katika shambulizi la eneo la Bryansk nchini Urusi asubuhi ya leo, wizara ya ulinzi mjini Moscow ilisema.

Makombora matano yalidunguliwa na moja kuharibiwa, huku vipande vyake vikisababisha moto katika kituo cha kijeshi katika eneo hilo, ilisema katika taarifa.

Matumizi ya makombora ya Marekani pia yaliripotiwa katika vyombo vya habari vya Ukraine, lakini Ukraine bado haijatoa maoni.

Matangazo

Katika taarifa, wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema shambuklizi hilo lilitekelezwa mwendo wa saa 03:25 (00:25 GMT).

Moto uliosababishwa na vifusi vilivyoanguka kutoka kwa moja ya makombora ulizimwa haraka na hakukuwa na majeruhi, ilisema.

Jeshi la Ukraine hapo awali lilithibitisha kwamba lilikuwa limeshambulia ghala la kuhifadhia risasi katika eneo la Urusi la Bryansk, lakini halikubainisha kama Atacms zilitumika.

Ilisema shambulio hilo kwenye ghala karibu kilomita 100 kutoka mpaka karibu na mji wa Karachev, lilisababisha milipuko 12 ya pili.

Vyombo vya habari vya Ukraine, vikinukuu chanzo cha kijeshi, viliripoti kuwa makombora hayo ya Marekani yametumiwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *