Na Polisi Kata ya Buguruni

Baadhi ya watu wanatupa madawa ya kulevya kwenye majalala kama vile bangi na mirungi, wakibainika kushughulikiwa kikamifu.

Hayo yamesemwa na Inspekta wa Jeshi la Polisi aliyekuwa akitoa elimu dhidi ya uharifu na ulinzi jirani kwa wafanyakazi wa Kanjenjere maeneo ya Buguruni Visiwani kwenye stendi ya mabasi yanayotoka Buguruni kwenda Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Inspekta Hadinan aliwapa elimu wafanyakazi wa Kajenjere kuwaambia kuwa waweze kulinda mitaa yao kama wanavyolinda ajira zao.

Aliwatahadharisha waweze kuangaliziana Mitaa Yao kipindi ambapo wapo kazini Ili kuhakikisha usalama wa familia na Mali zao.

Lingine aliwaomba wakiwa Kwenye kazi zao za kuzoa taka kuna watu huwa wanatupa mabaki ya mirungi au bangi hivyo watoe taarifa hizo kuwa katika taka za nyumba fulani walikuta hili na lile Ili Polisi washughulike nalo .

Aidha aliwakumbushia kufuata sheria za Barabarani Ili kuepuka ajali zisizo za lazima sio Kwamba kisa wewe unaendesha gari la taka Sheria itakaa kimya kwako.

Inspekta Hadinan amekuwa akitoa elimu ya ulinzi shirikishi katika jamii kwenye maeneo ya Buguruni akiwataka watu kuhakisha wanalinda maeneo kama jitihada za jeshi hilo kutoa elimu ya kutosha ya ulinzi shirikishi kwa umma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *