Jengo lililopo maeneo ya barabra ya Nyerere ambako kuna wateja wanatozwa malipo na DAWASA kwa huduma ya maji taka ambapo hakuna huduma ya kuunganisha maji taka
Na IBRAHIM KADILO
Licha ya kutokuwepo huduma ya kuunganisha mifumo ya maji taka barabara ya Nyerere, na baadhi ya maeneo mengi jijini Dar es Salaam, baadhi ya watu wanaendelea kulipia huduma hiyo Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Morningstar Post imebaini.
Uchunguzi wa Morningstar Post, umebaini kuwa watu wengi wameunganisha mifumo ya maji taka kwenye mifumo ya maji ya mvua na hivyo kutiririsha maji ya vyoo na kinyesi kwenye miundo mbinu ya barabara.
Kwa mujibu wa ‘Bill payments’ mteja mwenye jina la Ashby Ltd mwenye account number A10490088915 inaonesha analipa malipo ya huduma ya kuunganishiwa maji taka na Dawasa kwa miaka mitatu 2022, 2023 na mwaka huu.
Msemaji wa DAWASA, Bi. Everlasting Lyaro alipopigiwa simu kuthibitisha taarifa hizi, hakupokea simu yake, akaomba kutumiwa ujumbe kwenye simu yake ya mkononi.
Akijibu taarifa hizi kwa njia ya ujumbe wa maandishi, Bi. Lyaro hakukanusha taarifa hizi, alisema taarifa tulizomuuliza zimepokelewa na timu ya maji taka itazifanyia kazi kuthibitisha.
“Tumepokea na team ya Majitaka inaenda site kujiridhisha na taarifa hizi,” aliandika ujumbe Bi. Lyaro.
Akaongeza kuwa taarifa hizo zitakapokuwa tayari ingawa hakusema lini atamtaarifu mwandishi wa habari hizi.
Tatizo la watu kujiunganishia maji taka ya vyoo kutoka kwenye majengo, viwanda kwenda kwenye mifumo ya maji ya mvua limekuwa ni sugu na kero kubwa kwenye uchafuzi wa mazingira.
Baadhi ya wakazi wa jiji walihojiwa katika maeneo tofauti ambako hakuna mifumo ya maji taka walionesha kusikitishwa sana na kutokuwepo kwa mifumo ya maji taka katika maeneo ya katikati ya mji.
Wengi waliohojiwa wanasema karibu nusu ya watu wote wameunganisha mifumo ya maji taka kwenye mifumo ya maji ya mvua kwa sababu hakuna miundo mbinu ya maji taka na gharama ya kunyonya maji taka ni kub