NA MWANDISHI WETU
Mgomo wa wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama Wamachinga jijini Dar es Salaam, unaashiria nini?
Wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu wamachinga katika Soko la Simu2000, katika manispaa ya Ubungo, ijini Dar eS Salaam liingia kwenye mgomo asubuhi na kufunga barabara.
Wamachinga hao wanalalamikia mpango wa kukabidhiwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), sehemu ya eneo lao kwa ajili ya kujenga karakana ya mabasi yake.
Mbali na kufunga biashara zao, pia wameweka vizuizi katika barabara kuelekea Sinza na kuzuia magari kuingia na kutoka katika kituo hicho cha daladala.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko alifika eneo hilo na polisi, lakini wafanyabiashara hao walimtaka aondoke.
Mgomo huu umekuja wiki chache tangu kumalizika kwa mgomo wa kufunga biashara uliofanywa na wamiliki wa maduka katika soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam, na kuenea katika mikoa mengine, wakilalamikia mrundikano wa kodi
Migomo hii inaashria nini kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali ya mtaa na ule uchaguzi mkuu.
Tafsiri ya haraka ya kuwepo kwa migomo ya mara kwa mara ni kutoridhishwa kwa wananchi na sera na usimamizi wa utendaji wa viongozi walioko kwenye maeneo husika.
Katika hali kama hiyo serikali ya CCM inapaswa kujtazama upya kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali ya mitaa ambako ndio chimbuko la uimara na uthabiti wa msingi wa chama cha mapinduzi.