Na Mwandishi Wetu, Mbeya

WAKULIMA kutoka Kijiji cha Mbuyuni wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro wao dhidi ya wafugaji ambao umesababisha vijana wao kucharazwa fimbo na wafugaji baada ya mifugo yao kushikiliwa na wakulima kwa madai ya kuwa mifugo hiyo imekula mazao yao.
Wakizungumza na Waandishi wa Habari, wakulima hao wamesema baada ya kuikamata mifugo hiyo na kuamua kuishikilia wafugaji waliamua kuwavamia wakulima ambao kwa wakati huo walikuwa uwanjani wakicheza mpira na kuanza kuwapiga huku wakiwatishia kipigo baadhi ya wananchi waliokuwa wakiamuru mifugo hiyo itolewe shambani.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mbarali   Kanali Denis Mwila amekiri kuwepo kwa matukio ya migogoro ya ardhi inayotokana na wafugaji kuwatishia wakulima na kuwataka wananchi watakaovamiwa na kupigwa kutoa taarifa Jeshi la Polisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *