Hayati Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi

Na Mwandishi Wetu

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Hayati Mzee  Ali Hassan Mwinyi anazikwa visiwani Zanzibar, akiwa atakumbukwa kwa mengi aliyofanya wakati wa uhai wake.

Mzee Mwinyi amefariki dunia saa 11 jioni ya leo Alhamisi Februari 29,2024 katika Hospitali ya Mzena, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, kwa ugonjw  wa saratani ya mapafu iliokuwa unamsumbua.

Taarifa za kifo cha Mzee Mwinyi maarufu kama Mzee Ruksa, ziitangazwa Ikulu jijini Dar es Salaam na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mwinyi anazikwa nyumbani kwake Mangapwani visiwani zanzibara na viongozi mbalimbali wa kitaifa wamehudhulia mazishi yake.

Mzee Mwinyi anazikwa huku akikumbukwa na watanzania kwa mchango wake mkubwa alifanya kwa taifa kwa kipindi chote cha uongozi wake.

Mwinyi atakumbukwa na wengi kwani alikuwa Rais wa pili wa Tanzania alieongoza kwa kipindi cha miaka kumi kuanzia mwaka 1985 hadi 1995 huku akiwa ni rais wa kwanza kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia baada ya utawala wa chama kimoja.

Sera na falsafa ya mzee Mwinyi iliyompatia jina maarufu la Ruksa , itakubwa sana miongoni mwa watanzania wakati wa utawala wake aliweza kufungua mipaka ya uhuru wa maamuzi kwa watanzania kufanya kazi na biashara bila kuwekewa mipaka.

sera zake za kukaribisha uwekezaji ambazo zilileta unafuu wa maisha baada ya nchi kuwa imetoka kwenye vita vya kagera.

Mzee Mwinyi alipokuja na sera yake ya kufungua madirisha na milango basi kila mkopo ukaingia vizuri na tukapata nafuu tofauti na kabla ya hapo, hiyo ni kuonyesha tu kwamba aliingia kipindi kigumu na akafanya kazi na Watanzania hawamsahau kwa hilo ndio maana wanamuita Mzee rukhsa.

Mzee Mwinyi atakumbwa kwa mengi kwai ndiye Rais aliyetuingiza katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, na ndiye alietuondoa katika mfumo wa kiimla wa chama kimoja. Tanzania ni nchi ya vyama vingi sasa hivi kwa sababu ya Mzee Mwinyi, ilitokea wakati wa urais wa Mzee Mwinyi,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *