Na Mwandishi Wetu

KLABU ya Simba SC, imefungiwa kusajili wachezaji mpaka itakapolipa madai ya timu ya Teungueth ya Senegal kuhusu mcheza Pape Ousmane Sakho.

Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya klabu hiyo kushinda kesi ya madai dhidi ya Simba kutokana na mauzo ya Sakho. 

Kabla ya kujiunga na Simba, Sakho ambaye hivi sasa anachezea timu ya Quevilly Rouen Metrapole ya Ufaransa, alikuwa mchezaji wa Simba.

Klabu hiyo ilifungua kesi FIFA dhidi ya Simba ikidai sehemu ya malipo kutokana na mauzo ya Sakho. Simba ilitakiwa iwe imetekeleza uamuzi huo ndani ya siku 45 tangu ulipotolewa lakini haikufanya hivyo.

“Wakati FIFA imeifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeifungia Simba kufanya uhamisho wa ndani,” ilieleza sehemu ya taarifa ya TFF kuongeza.

“TFF inazikumbusha klabu kuheshimu sharia, kanuni na taratibu za mpira wa miguu ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili wachezaji,” ilimaliza taarifa hiyo.

Wakati taarifa hiyo ikiwafikia Simba, uongozi wa klabu hiyo umekiri kudaiwa, lakini wakieleza ilikosekana mawasiliano bora kwa pande zote mbili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *