Na MWANDISHI WETU
GWIJI wa muziki wa dansi nchini Kamarade Ally Chocky anakuja na Extra Bongo kwa awamu ya tatu na safari hii itakwenda na kauli mbiu ya “Baba Lao”.Awamu ya kwanza alianza na wimbo 3×3, awamu ya pili akaanza na “Mjini Mipango”.
Awamu zote mbili za Extra Bongo zilifanya vizuri sana lakini bado bendi ikashindwa kuhimili mawimbi ya soko la dansi na kufa kifo cha kawaida.Awamu hii ya tatu Chocky ameiambia Morning Star Post kuwa atakomaa nayo mpaka mwisho na ndio maana ameamua kuiita Extra Bongo Baba Lao.
“Nimejipanga vizuri mno, nimefanya utafiti wa kutosha kabla ya kuiunda upya Extra Bongo,” alisema Chocky katika mazungumzo yake na mtandao huu.Katika kudhihirisha kuwa safari hii Chocky amejipanga vilivyo, anakuja na wimbo “Penalti ya Mwisho” ambao utakuwa na ujumbe uliobeba maono makubwa.
Wimbo “Penalti ya Mwisho” ndio utakaokuwa kete ya kwanza ya awamu ya tatu ya Extra Bongo.Nyimbo nyingine nyingi mpya alizonazo Ally Chocky kwaajili ya Extra Bongo ni pamoja na “Kinyago Changu”, “Pambana na Hali Yako” na “Tatiana Kumba
Ally Chocky Gwiji la Muziki wa Dansi, Mzee wa Farasi