Na Mwandishi Wetu

KAMA unafikiri Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, ameridhika na upana wa kikosi cha timu hiyo basi utakuwa unakosea sana.

Licha ya kwamba timu yake iko kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara, pia ikiwa na uhakika wa kulitetea taji la FA, bosi huyo bado ana kiu ya kufanya makubwa zaidi, hasa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga imeshatinga hatua ya makundi lakini Injinia Hersi anaona bado kikosi hicho cha kocha Miguel Gamondi kinahitaji kufanyiwa marekebisho ili kukiimarisha zaidi.

Taarifa za ndani, Rais huyo anataka kuona Yanga ikifika walau nusu fainali ya michuano hiyo ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Sasa, kwa mujibu wa chanzo chetu  benchi la ufundi limeshaandaa ripoti yake fupi ya usajili na kuikabidhi kwa Injinia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *