BINGWA wa WBC Afrika na bondia namba moja nchini, Fadhili Majiha ameweka rekodi ya kuwa bondia wa kwanza kupata hadhi ya nyota nne na nusu katika viwango vya ngumi duniani (boxrec) tangu nchi ipate uhuru.

Aidha, Majiha amevunja rekodi ya bondia, Hassan Mwanyiko na Tony Rashid katika mtandao wa boxrec.
Majiha ameweka rekodi hiyo baada ya wiki iliyopita kushinde mkanda wa ubingwa wa Afrika kwa kumchapa kwa pointi Bongani Mahlangu wa Afrika Kusini katika pambano la raundi kumi ambalo lilipigwa kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba, jijini Dar es Salaam.

Bondia huyo mwenye asili ya mkoa wa Lindi Wilayani Ruangwa, mbali ya kufikisha nyota hizo nne na nusu, lakini ameingia katika orodha ya mabondia 10 bora duniani akiwa kwenye nafasi ya saba kati ya 1056 wa uzani wa Bantam.

Ikumbwe kuwa bondia Mwakinyo ndiye bondia wa kwanza nchini kufikia hadhi ya nyota nne pamoja na kuingia kwenye 10 bora ya dunia uzani wa Super Walter kwa kukaa katika nafasi ya tisa kabla ya Tony Rashid kufikisha nyota tatu na nusu na kuingia kwenye 20 bora ya dunia ya uzani wake wa Super Bantam yenye mabondia 1248.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *