Na AFP

Jenerali Abdourahmane Tchiani amejitangaza kuwa kiongozi mpya wa Niger baada ya mapinduzi makubwa.

Jenerali Abdourahmane ambaye pia anajulikana kama Omar Tchiani, aliongoza mapinduzi ambayo yalianza Jumatano wakati kitengo cha walinzi wa rais alichoongoza kilimkamata kiongozi wa nchi.

Hii inatatiza kipindi cha kwanza cha mpito cha amani na kidemokrasia nchini Niger tangu ijinyakulia uhuru wake mwaka 1960.

Rais Mohamed Bazoum anadhaniwa kuwa katika afya njema, na bado anashikiliwa na walinzi wake.

Kikosi cha wanajeshi 700 kilianzishwa na mtangulizi wa rais aliyepinduliwa Mahamadou Issoufou kulinda dhidi ya utekaji wa kijeshi.

Alihusishwa na jaribio la mapinduzi ya 2015 dhidi ya Bw Issoufou.Kesi iliyofuata kortini mnamo 2018 ilimuondolea makosa ya kuhusikaKabla ya kuchukua mamlaka ya kijeshi,Rais Bazoum alikuwa amepanga kumuondoa jenerali huyo kama sehemu ya mabadiliko aliyokuwa akiyafanya kwa vikosi vya usalama, gazeti binafsi la Niger la L’Enqueteur linaripoti.

Jenerali Abdourahmane Tchiani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *