Na Reuters
Kiongozi wa mamluki wa Wagner, Yevgeny Prigozhin, amekaribisha mapinduzi ya kijeshi nchini Niger, kulingana na ujumbe wa sauti ambao haujathibitishwa.
Niger imekuwa mshirika mkuu wa Magharibi katika vita dhidi ya wanamgambo wa kijihadi katika eneo la Afrika Magharibi.
Marekani na Ufaransa, ukoloni wa zamani zina kambi za kijeshi katika nchi hiyo yenye utajiri wa madini ya uranium.
Ujumbe wa sauti ambao haujathibitishwa kutoka kwa Bw Prigozhin ulioibuka kwenye mtandao wa Telegram inayohusishwa na kundi hilo, ikisema kuwa mapinduzi hayo yalikuwa yamechelewa.
Kulingana na shirika la habari la Reuters, mzungumzaji huyo alikuwa na matamshi ya lugha ya Kirusi na sauti kama mkuu huyo wa Wagner.
“Kilichotokea Niger si chochote zaidi ya mapambano ya watu wa Niger dhidi ya wakoloni, ambao walijaribu kuweka sheria zao za maisha,” shirika la habari la AFP linamnukuu akisema.
“Ili kudumisha mfumo wao halisi wa utumwa katika maeneo ya mataifa haya, wanapeleka vikosi mbalimbali za kigeni, ambavyo vinafikia maelfu ya askari.”
Aliendelea kusifu “ufanisi” wa Wagner, akielezea maelfu ya wapiganaji wake “wanaweza kurejesha utulivu na kukabiliana na magaidi, kuwazuia wasidhuru raia”, AFP inaripoti.
Kutolewa kwa ujumbe wa sauti kuliendana na kuchapishwa kwa picha kwenye Telegram zinazomuonyesha Bw Prigozhin huko St Petersburg katika mkutano wa kilele wa Afrika na Urusi.
Alionekana akipeana mkono na Balozi Freddy Mapouka, afisa mkuu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).
Ni mara ya kwanza kuthibitishwa kuonekana kwa Bw Prigozhin nchini Urusi tangu Wagner waliposhindwa kufanya uasi wao dhidi ya Urusi mwezi Juni.
Wagner ina mkataba wa usalama nchini CAR na kupitia mtandao wake wa makampuni yanayodaiwa kufanya biashara huko katika migogoro ya madini na mbao, pamoja na kutengeneza bia na vodka.
Kundi hilo la mamluki pia liko nchini Mali, ambako linaaminika kuwa na wanajeshi wapatao 1,000 ambao wameshutumiwa kutekeleza ukatili.
Kutumwa kwao mwezi Disemba 2021 kulifuatia kuvunjika kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya utawala wa kijeshi wa Mali na Ufaransa, na kusababisha ukoloni wa zamani kuwaondoa wanajeshi wake wa kukabiliana na ugaidi.
Kulingana na Reuters, kiongozi huyo wa Wagner alisikika kwenye video iliyotolewa mapema mwezi huu akiwaambia wapiganaji wake, ambao sasa wamehamishwa Belarus, kwamba wanapaswa kuimarisha nguvu zao kwa “safari mpya ya Afrika”.
Kiongozi wa mamluki wa Wagner, Yevgeny Prigozhin,