Na DW

Mwishoni mwa mwezi Juni, Wizara ya Kuamrisha Mema na Kuzuia Maovu ilitoa muda wa mwisho wa hadi leo kwa saluni zote kufungwa na kusema muda huo ungewezesha wafanyabiashara hao kumaliza matumizi ya bidhaa zilizobakia.

Wizara hiyo imesema ilitoa agizo hilo kwa sababu pesa nyingi zinazotumika kwa urembo zinasababishia hali ngumu kwa familia maskini na kwamba baadhi ya huduma katika saluni hizo haziendani na maadili ya Kiislamu.

Mamlaka hiyo imeongeza kuwa vipodozi vingi vinawazuia wanawake kutawadha vizuri kwa ajili ya sala huku kuongeza kope na kusuka nywele pia kukipigwa marufuku.

Nakala iliyoonekana na shirika la habari la AFP, inasema maagizo hayo ya mdomo yanatoka kwa kiongozi mkuu, Hibatullah Akhundzada.

Salon za urembo nchini Afghanistan

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *