Na Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Mapato Nchini TRA, inachunguza kampuni tatu za ulinzi zinazodaiwa kuuzwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kisutu Bw Mustaquim Darugar kwa mamilioni ya shilingi bila kulipa kodi ya mapato.

Akizungumza na Morningstar Post, Afisa Mahusiano wa (TRA), Bw. Avitus Rushaka, alisema kuwa TRA haiwezi kuthibitisha taarifa za kampuni hizo kwa sasa uchunguzi utakapo kamilika

Aliongeza kuwa taarifa hizo zinatakiwa kupelekwa kwenye idara ya uchunguzi wa kodi  na kufanyiwa kazi.

Alisema idara yake ya elimu kwa mlipa kodi haiwezi kutoa majibu ya taarifa za kampuni hizo zinazodaiwa kuuzwa na Darugar bila kulipa kodi ya mapato (Capital gain tax ) mpaka pale yatakapochunguzwa na kutolewa taarifa rasmi.

“Taarifa hizi za kuuzwa kwa kampuni zipelekwe kwenye idara husika halafu sisi tutafuatilia kuthibitisha kuwa zimefanyiwa kazi na kutoa taarifa kwenu zikiwa zimethibitishwa kwa sasa hatuwezi kusema lolote kuhusu taarifa hizo,” alisema Bw Rushaka

Bw Darugar anadaiwa kukosesha serikali mapato kwa kuuza kampuni bila kulipa kodi ya mapato (capital gain).

Pia, anadaiwa  kunyanyasa wafanyakazi wake kwa kuwafukuza kazi bila kuwalipa stahiki zao na kuuza kampuni pamoja na wafanyakazi bila kufuata taratibu.

Anadaiwa amesajili makampuni ya ulinzi na kuyauza kwa watu wengine bila kufuata taratibu na kulipa kodi ya mapato (capital gain).

Kampuni zinazotaiwa kusajiliwa na mwenyekiti huyo ni Simply Safe Security, Stay Alert Stay Safe Security , (ASASS), Power Sheld Security, Simply Safe Security na Thinkx GSM Security ambayo bado anaendelea kuiendesha mwenyewe.

Kampuni ya ASASS imeuzwa kwa bwana Ali Jawadu ambaye mauziano hayo hakuna mapato ya kodi yaliyolipwa serikalini na kampuni hiyo inaendeshwa na Jawadu mtaa wa Kitonga ambako ofisi zake zilipo.

Kampuni hiyo inaendeshwa na Jawadu baada ya kununua kutoka kwa Bw Darugar.

Kampuni nyingine za ulinzi zilizouzwa na Darugar ni Simply Safe Security iliyouzwa kwa Bw Abdala, na mwingine anayefahamika kwa jina la Macho ya Paka na Almin Murtaza ambaye ni mtoto wa bw Darugar.

Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi za Darugar waliohojiwa na Morningstar Post wameonesha wasiwasi na mashaka kuhusu ajir zao kwa kampuni kuuzwa wakati wakiwa na mikataba na Darugar.

Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Simply Security anayedaiwa kuwa ni mtoto wa Darugar alipoulizwa hakutaka kuzungumza lolote na kutaka andikiwe barua rasmi ya kuulizwa mambo kuhusu tuhuma hizo.

Wakizungumza kuhusu kampuni za Darugar ya Thinkx GSM Security, baadhi ya wafanyakazi ambao hawakupenda kutajwa majina yao walisema kuwa hakuna hata mfanyakazi mmoja mwenye mkataba wa ajira wala kusajiliwa kwenye mfuko wa Fidia za Wafanyakazi (WCF).

Wafanyakazi wa Darugar ambao hawana mikataba ya ajira ni pamoja na Baraka, Juma Ingo, Jeff Masabala ambao ni askari wa tahadhari (rapid rider).

Wengine ni Goshet Nyerere, Amon Rafael, Peter na Jakson ambao ni operasheni meneja. Pia, David na Shaff wataalam wa masuala ya IT, ambao hawana mikataba ya ajira.

Awali akijubu tuhuma hizo, Bw Darugar alimjia juu mwandishi wa Morningstar POST na kumtisha kuwa yeye ni mtu wa serikai yuko kwenye system na majina yake yako katika watu walioko ikulu anafahamika hivyo hatishi na mwandishi.

Alisema kuhusu kampuni zake vibali vyote anavyo na anawafanyakazi nane tu kwa kuwa yeye anahusika na kufunga alam za ulinzi tu na mikataba kwa wafanyakazi wake ipo michango ya NSSF na WCF yote anakata.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *