Wakazi wa Kata ya Pugu maeneo ya Kigogo Freshi, wilaya ya Ilala, Jijini Dar es Salaam, kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakikabiliana na adha ya dimbwi kubwa la maji machafu lililoko maeneo ya stendi ya mabasi karibu kabisa na soko la maeneo hayo.
Licha ya mvua zinazoendelea kunyesha kuzidi kuathiri eneo hilo, kwa muda, mrefu sana wakazi wa maeneo hayo wanasema dimbwi hilo limekuwepo hapo na viongozi kata na jimbo wamekuwa wakitua dimbwi hilo kama kigezo cha kuombea kura.
Viongozi hao wakichaguliwa hakuna anayehangaika tena kuondoa kero hiyo kila mwaka.
